Rais ashauriwa jambo na NIKKI MBISHI....soma zaidi


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nikki Mbishi amemtaka Rais John Pombe Magufuli kutupia jicho katika mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART)  ambapo amedai asipofanya hivyo kuna uwezekano mkubwa mradi huo ukafa bila kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, ‘Dada Pumzisha Mwili Wako’ amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuona mapungufu kutoka kwenye mradi huo ambapo ma -bus yamekuwa yakijaza idadi kubwa ya watu na kudai ni kupitiliza kiwango kilichokusudiwa.

“Hadhi ya mwendokasi ni ‘level seat’ siyo kushonana kama embe toka kibada.  Mzee Magufuli tazama hilo, mradi unakufa ‘soon’. Mwendokasi watu wanajazana kama ‘3rd class train’ ya India yatadumu kweli ?” 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Baada ya Kumwagana na Ali Kiba,,Jokate Aaamua Kuweka Wazi Vigezo kwa Kidume Mwingine Anayemtaka..!!!

Mimi Mars Amkana Dada Ake Vanessa Mdee...Asema....