Raisi kutinga leo Tanga.
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kesho kwa ziara ya kikazi ambayo pamoja na mambo mengine, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Bandari ya Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amebainisha hayo jana wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais Magufuli pamoja na mgeni wake, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Shigella alisema kimsingi maandalizi yote muhimu kuhusu ziara hiyo yamekamilika na kwamba Rais Magufuli atawasili mkoani Tanga na kupokewa wilayani Handeni katika mji wa Mkata ulioko pembezoni mwa barabara kuu ya Segera- Chalinze
Maoni
Chapisha Maoni