Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2017

Goood News!!! Rayvanny ameshinda tuzo ya BET 2017

Picha
Staa wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka WCB ameshinda tuzo ya BET kipengele cha Viewers Choice Best New International Act Artist. Alichokiandika Diamond Platnumz baada ya Rayvanny kushinda tuzo ya BET 2017 kama ‘ Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah!  ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!!  @babutale ‘ ‘ THE BET Viewers Choice Best New International Act 2017 !!!!!!!!!!!!! WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike  @Wcb_Wasafi  TANZANIA!!!! Chkua hiyo   #Wcb_Wasafi   #WinningTeam !’

hongera Rayvanny

Picha

Young Killer Msodoki Amdissi Nay Wa Mitego(Nay True) Kwenye Wimbo Huu. TRUE BOYA BY YOUNG KILLER

Picha

EXCLUSIVE:Rayvanny Baada ya Kushinda BET Awards Viewers Choice Best International Act Award 2017

Picha

Diamond Platnumz kaongea baada ya Rayvanny kushinda Tuzo ya BET

Picha

NEW (OFFICIAL VIDEO) Rayvanny-Mbeleko

Picha
(OFFICIAL VIDEO) Rayvanny-Mbeleko

Hawa Hapa Waliochaguliwa Kidato cha Tano, Wanafunzi 3,000 Waliofaulu Waachwa..!!!

Picha
Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku wanafunzi 2,999 wakiachwa. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene ametoa idadi hiyo leo Juni 9, mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Amesema kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 pekee waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Amesema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu kwa vigezo vyote vya msingi ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima. Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na ki...

Wabunge wa CCM na Upinzani Watofautiana Kuhusu Bajeti ya Serikali...!!!

Picha
Wabunge wa CCM wameipongeza bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 wakisema inalenga kuondoa kero za wananchi wa hali ya chini huku wenzao wa upinzani wakisema ni bajeti ya maumivu kwa watu wa hali ya chini baada ya mafuta kuongezeka. Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti mara baada ya bajeti hiyo kusomwa bungeni jana, wabunge wa CCM walisema bajeti hiyo imemaliza kila kitu. Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hilaly alisema bajeti hiyo imekidhi matakwa ya wabunge ingawa bado hawajafahamu wananchi wataipokea vipi. “Kimsingi yale tuliyokuwa tunayapinga mwaka jana, mwaka huu wameyaondoa. Nataka nimpongeze waziri ameleta bajeti nzuri sana tumeipokea kwa mikono miwili. Kazi iliyobaki ni kwenda kuipitia ili maeneo ya kurekebisha tufanye hivyo. Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa alisema katika kipindi cha miaka 15 aliyokuwa ndani ya Bunge haijawahi kutokea bajeti nzuri iliyowalenga wananchi wa chini kama ya mwaka huu. “Kwa mfano maeneo ya kodi katika mazao ya wak...

Lulu Michael Amzimikia Mwanamuziki Aslay...Adai Ndio Mfalme Wake

Picha
Kupitia mtandao wa Twitter wa Mwandada huyo ameonesha mapenzi ya wazi wazi ya ushabiki wake kwa Mwanamuzili Aslay kwa kuandika "Aslay ni Mfalme wangu wa Bongo Fleva🙌🏿🙌🏿 Ni Moto🔥Anaunguza🔥🔥🔥🔥🔥🔥" Lulu amezitaja nyimbo 3 za Aslay alizoachia hivi karibuni na kusema zote ni kali.

Soda, bia, petroli,sigara, mvinyo wa nje bei juu.

Picha
SERIKALI imetangaza kufuta ada ya leseni ya magari, kupandisha bei ya vinywaji baridi na bia, mafuta na kupunguza ushuru wa mazao unaotozwa na halmashauri za wilaya kutoka asilimia tano hadi tatu. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitangaza hayo jana wakati akisoma Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni mjini hapa. Akizungumzia Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, alisema kuwa serikali inafanya marekebisho ya viwango maalumu vya ushuru kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa kiwango cha mfumuko wa bei cha asilimia tano. Hata hivyo, Dk Mpango alisema kwa kuzingatia Mkakati wa Taifa kukuza uchumi wa viwanda, baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini hazitafanyiwa marekebisho hayo. Dk Mpango alieleza kuwa ushuru wa bidhaa kwenye viwanja baridi unapandishwa kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 kwa lita ikiwa ni ongezeko la Sh tatu kwa kila lita. Aidha, ushuru wa bidhaa kwenye maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye chupa yaliyoagizwa kutoka nje kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 ...

BAJETI YA WANANCHI MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Picha
BAJETI ya pili ya Rais John Magufuli imeendelea kugusa maisha ya wananchi wa kawaida wa Tanzania baada ya kutangaza hatua kadhaa zilizojielekeza kuwaondolea mzigo na kuwafanya wawe na maisha bora. Bunge jana likiwa na karibu theluthi tatu ya wabunge wote, lilimkatisha kwa nderemo na vifijo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/18. Walifikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ambazo zimeonekana dhahiri zitawaondolea mzigo wananchi wa Tanzania. Ilifikia hatua Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliuliza kama awahoji wabunge kwamba Dk Mpango asiendelee na hotuba yake kwani bajeti hiyo imekidhi haja kubwa au kwa maneno ya mtaani “imefunika.” Miongoni mwa mambo mazuri ya bajeti hiyo ni kufuta ada ya kila mwaka ya leseni ya magari; kufuta ada ya ukaguzi wa viwango vya mazao ya biashara; kutoza kodi ya VAT kwa kiwango cha sifuri kwa huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje y...

Pwani yang'ara kwa miradi mipya

TANZANIA ya viwanda ni ndoto ambayo haina muda mrefu itatimizwa baada ya mwelekeo wa kujenga uchumi wa viwanda kuanza kuwa mzuri, na huku mifuko ya hifadhi ya jamii ikionesha nia ya kuwekeza katika miradi ya viwanda katika maeneo mbalimbali nchini. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema miradi ya viwanda mbalimbali imeanzishwa kutokana na mchango wa sekta binafsi katika mikoa mbalimbali nchini. Dk Mpango alikuwa akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka 2017/18. Alisema kwa mfano, Mkoa wa Pwani una jumla ya miradi mipya ya viwanda 82. Aliitaja baadhi ya miradi mikubwa ya viwanda iliyozinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi kwa mkoa wa Pwani pekee ni viwanda viwili vya Tywford Tiles (Chalinze) na Goodwill Ceramic (Mkuranga) vya kutengeneza marumaru (tiles); kiwanda cha nondo cha Kiluwa Steel Industries Ltd (Mlandizi Pwani) ambacho kimeanza uzalishaji; kiwanda cha Global Packaging (Mailimoja Pwani) ambacho kinafanya kazi....

Anachoamini Wema Sepetu kuhusu Rayvany na BET

Picha
Msanii  RayVanny  ndiye msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ambaye anatuwakilisha kwenye tuzo za muziki za  BET  zitakazofanyika nchini Marekani hivi karibuni. RayVanny amechaguliwa kuwania tuzo ya  Viewers Choice Awards  ama (Pendekezo la Mashabiki ama watazamaji) na  BET  wametangaza namna ya kuwapigia kura wasanii ili washinde tuzo hizo . Pamoja na baadhi ya mastaa kama  Elizabeth Michael  kumpigia na kumuombea  kura  RayVanny  kura kwenye kurasa zao za Social media  ,  Wema Sepetu  naye ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpigia kura RayVanny kwa kuandika>>> Umechaguliwa tu kuwania lakini kwangu wewe ni mshindi tayari …Unastahili kabisa! V-Vanny Boy. Na haiishii hapa Tuendelee kupiga kura.   Wasanii wanaowania tuzo ya Viewers Choice Awards pamoja na  RayVnanny  ni pamoja na   Dave (UK ) Jorja Smith (UK) Amanda Black (South Africa) Changmo (...