Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

HESLB YATOA MWONGOZO NA VIGEZO VYA UTOAJI MIIKOPO KWA MWAKA 2017/2018

Picha
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 na itaanza kupokea maombi ya mikopo kuanzia tarehe 6 Agosti 2017 hadi tarehe 4 Septemba, 2017. Waombaji wote wa mikopo watarajiwa mnasisitizwa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 pamoja na taratibu nyingine za uombaji mkopo kabla ya kujaza fomu za maombi ya mkopo zinazopatikana kwenye mtandao wa  https://www.heslb.go.tz Kusoma mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 bofya hapa   Kusoma hatua za kufuata kufanya maombi ya mkopo na malipo bofya  hapa Kusoma kuhusu sifa za msingi za mwombaji kwa Kiswahili bofya hapa     na kwa Kiingereza bofya  hapa  

Magufuli atoa yaliyomoyoni-Adai Mwizi ni Mwizi tu Hata Kama ni Mzungu

Picha
RAIS John Magufuli amesema ifike wakati wizi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya viongozi wa serikali wakishirikiana na wawekezaji kutoka nje ukomeshwe ili kuleta maendeleo ya Tanzania kwa ajili ya wananchi wote na si watu wachache kujinufaisha. Hayo ameyasema leo wakati akiwahutubia wanachi wa Hale wilayani Korogwe wakati akianza ziara yake ya siku tano mkoani Tanga ambapo atashirikiana na Rais Museveni wa Uganda kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani kwenye mwambao wa bahari ya Tanga, Agosti 5 mwaka huu. “ Mlinipa kura nyingi sana na ninawashukuru na ahadi yangu iko palepale kwamba sitawaangusha, unapokuwa na kiongozi anayewatumikia wananchi ni jambo nzuri." “Hatukuumbwa kwa ajili ya kuwa wasindikizaji wa watu bali tumeumbwa ili kuwa Tanzania yenye neema ndiyo maana hata kwenye kutumbua majipu huwa sijali hata kama ni Mzungu. Wapo Wazungu waliokuwa wamezoea kutumbua dhahabu yetu, nimeamua kuwatumbua bil...

MSEMAJI wa Simba Haji Manara Azidi Kutoa Tambo Dhidi ya Yanga..Adai Mwaka Huu ni wa SIMBA

Picha
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kusema kuwa mwaka huu lazima Simba itachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kuvunja utamaduni wa Yanga kuchukua kombe hilo mfululizo. Haji Manara amesema hayo leo wakati wa hafla ya kukabidhi jezi na vifaa vya michezo kwa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara 2017/2018 iliyoandaliwa na mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara Mbali na hilo Manara aliomba fedha ziwe zinawaishwa kidogo ili kuweza kusaidia vilabu vingine vidogo ambavyo vinachangamoto kubwa ya mapato ili kusaidia vilabu hivyo kufanya maandalizi kwa wakati. "Tuangalie hizi timu za mikoani zinapata changamoto nyingi sana tuombe pesa zitoke kwa wakati ili timu ziweza kupanga bajeti zao za usafiri na mambo mengine lakini niseme tu mwaka huu Simba lazima ishinde ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2017/2018" alisema Haji Manara Klabu ya Simba imeshindwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu minne sasa huku watani wao wa jadi Yanga wakichukua ubingwa huo ma...

KIMENUKA...Kufuatia Kumruhusu Mtoto Kurusha Ndege, Kibarua Cha Marubani Chaota Mbawa

Picha
MTOTO AKIRUSHA NDEGE Serikali nchini Algeria, imewafukuzwa kazi marubani wawili wanaofanya kazi katika shirika la ndege la serikali baada ya kumruhusu mtoto wa miaka 10 kuendesha ndege. Mtoto huyo anayedaiwa kuwa ni yatima alikuwa akiendesha ndege aina ya Air Algerie, iliokuwa na abiria ndani na ilifanya safari zake katika mji wa Algiers hadi Setif. Zoezi la mtoto huyo kuendesha ndege lilifadhiliwa na kurekodiwa kituo cha El Bilad TV, ambapo walionyesha tukio zima huku kijana huyo akiwa amevalia sare za rubani. Baada ya video na picha kusambaa za kijana huyo akiongoza ndege, ndipo serikali ilichukua hatua ya kuwafukuzwa kazi Marubani hao mnamo Julai 29 mwaka huu.

UHAMISHO Neymar Utata Mtupu....La Liga Yagoma Kumuachia Wanasheria Wavamia

Picha
Shirikisho la soka nchini Hispania limeingilia kati usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazili, Neymar Dos Santos kujiunga na Paris Saint-Germain kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 198 kiasi ambocho kinamfanya kuweka rekodi ya dunia akitokea Barcelona. Zikiwa zimesalia saa chache kuhitimisha kwa usajili huo wa Neymar kumeibuka wingu zito katika usajili huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya dunia, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema PSG walishajaribu kutuma dau hilo kwa Barcelona ili kujaribu kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo lakini La Liga walikikataa kiasi hicho cha pesa. Uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar umepingwa vikali na La Liga huku ikigomea sheria inayotumika kumsajili mchezaji huyo Wanasheria wa PSG wamewasili katika shirikisho hilo (La Liga) mjini Madrid  leo  Alhamisi katika kuhakikisha wanazima jaribio la La Liga kumzuia mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 25 .

Ni kweli aliyekuwa mke wa Nuh Mziwanda ameolewa na mwanaume mwingine? Nuh kaandika haya

Picha
Baada ya kusikika kwenye Uheard ya August 2, 2017   waliokuwa wanandoa Nuh Mziwanda na Nawali wanaodaiwa kutengana baada ya kutoishi karibu kama awali huku Nuh Mziwanda akidaiwa kurudi kwenye dini yake ya zamani. Kwenye Uheard hiyo wote walisikika wakilaumiana japo Nawali alinukulika akisema kuwa  “Nuh   kashantoka nina mume mwingine kwani hamna habari..? mume wangu hataki mambo ya nini nini.”  Sasa Leo August 3, 2017 kwenye ukurasa wa Instagram wa Muimbaji Nuh Mziwanda amepost maneno yanayoashiria kuwa  Nawal  ameolewa na mtu mwingine baada ya ujumbe wa kumpongeza na kumtakia maisha mema yeye na mume wake huyo mpya huku Nawal akifuta picha zake zote alizokuwa amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram….

IDEO: Ben Pol afunguka ya Ebitoke kumlipa Milioni 3

Picha
Msanii wa muziki Ben Pol amekanusha taarifa ambazo zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba alilipwa tsh milioni 3 na uongozi wa Timamu Media ili afanye kiki na mchekeshaji, Ebitoke. Muimbaji huyo amedai kila kitu ambacho kimetokea kwenye maisha yake akiwa na Ebitoke hakuna Kilichotengezwa huku akidai yote yalikuwa ni maisha yake halisi. SIKILIZA HAPA

R Chuz Naye Afunguka Kuhusu Hali ya Jini Kabula

Picha
Mwigizaji Tuesday Kihangala ambaye ni mzazi mwenza na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye kwa sasa yupo kwenye matatizo, amezungumzia hali anayokabiliana na mwigizaji huyo na kuonesha kusikitishwa kwake ingawa wameachana. Akionesha kuumizwa na hali iliyomkuta Jini Kabula, Tuesday amesema yupo karibu na familia yake na kuwapa ushirikiano kuhakikisha wanamsaidia kwa hali na mali. ”Ni taarifa za kuumiza sana hata mtu yoyote hata kama huna mahusiano naye na siyo mzazi. Inaumiza sana kama binadamu, ingawa sipo Dar es Salaam lakini tuna mawasiliano mazuri wakati akiwa na nafuu na ninawasiliana vizuri na familia yake kuangalia namna gani tunaweza kutatua hili suala. Tulibahatika kuwa na mtoto mmoja toka mwaka 2007 ambapo tulivunja mahusiano.” – Tuesday Kihangala.

Raisi kutinga leo Tanga.

Picha
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kesho kwa ziara ya kikazi ambayo pamoja na mambo mengine, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Bandari ya Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amebainisha hayo jana wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais Magufuli pamoja na mgeni wake, Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Shigella alisema kimsingi maandalizi yote muhimu kuhusu ziara hiyo yamekamilika na kwamba Rais Magufuli atawasili mkoani Tanga na kupokewa wilayani Handeni katika mji wa Mkata ulioko pembezoni mwa barabara kuu ya Segera- Chalinze